Published by SAUTI YA UJAMAA
Lengo la Jukwaa hili ni kuendeleza nadharia na mapambano ya kupigania Ujamaa na Umajumui wa Afrika. Siku zote, na popote tunapokuwa, tunasimama upande wa wavujajasho. Tunaupinga ubepari katika sura zake zote (ubeberu, uliberali mamboleo n.k ) pamoja na mifumo mingine kandamizi inayostawisha ubepari (mfumo dume, ubaguzi wa rangi, ukabila, udini, ukaburu wa kiumri n.k ). Tunapambana kuibomoa mifumo hii yote ili kujenga mfumo unaozingatia uhuru, utu, haki na usawa.