By Gibson J.E Mdakama | August 2018
UTANGULIZI
Maktaba za umma ni moja ya vyombo muhimu sana katika ukuaji wa ubora wa elimu nchini. Umuhimu wa kuwa na maktaba za umma nchini kwa sasa umekuwa ni sehemu kuu ya mahitaji ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla katika kuhakikisha taifa linasonga mbele katika Maendeleo ya Elimu pamoja na uchumi wa nchi hasa kuifikia nchi ya uchumi wa viwanda kama tulivyojiwekea malengo hayo kupitia Sera ya Maendeleo ya nchi ya 2014/15-2024/25.